
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali akiwaaga wanafunzi wa Ufadhili wa Masomo nchini Rasilhema
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ally
Abdul Gulam amewataka wanafunzi waliopata bahati ya Ufadhili
wa Masomo nchini Rasilhema kuendendeleza nidhamu na bidii
katika kipindi chote watachokuwa masomoni ili kuweza kupata
matokeo mazuri katika masomo yao.
Hayo yameelezwa wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata
nafasi ya kuendelea na Masomo ya Digree ya kwanza
yaliodhaminiwa na Rasilhema hafla iliyofanyika katika ukumbi wa
mkutano waOfisi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Mazizini .
Amesema ni vyema wanafunzi hao kuitumia fursa ya udhamini
walioipata ya kwenda kusoma nje, kwani kutawasaidia kuengeza
elimu ambayo wataweza kuja kuitumia katika kuliendeleza taifa
hivyo amewasihi kwenda kuendeleza nidhamu na maadili katika
kipindi chote cha masomo yao.
Ameeleza kuwa Serikali ya Mapindunzi ya Zanzibar na Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania imekuwa ikichukuwa jitihada katika
kuhakikisha inaimarisha miundombinu bora kwa wanafunzi ili
kuwawezesha kuendelea na elimu ndani na nje ya nchi .
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw Iddi
Khamis Haji amesema wanafunzi 40 walipitia mchakato huo na
watano wamebahatika kupata ufadhili huo na wanatarajiwa
kuondoka hivi karibuni kwenda kuendelea na masomo ya Chuo
Nchini Rasilhema
Wanafunzi wanaliopata nafasi hiyo Said Ali Hamadi na Zulfa
Rashid Gharib wameipongeza serikali kwa kuibua fursa mbali
mbali za masomo nje ya nchi hivyo wameahidi kwenda kusoma
kwa bidii ili kuweza kuja kuendeleza taifa