News

TANGAZO MAALUM KWA WALITEULIWA KUPATA MIKOPO AWAMU YA PILI

2021-11-10 13:54:13.0

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR (BMEJZ) INATANGAZA MAJINA YA WAOMBAJI WALIOTEULIWA KUPATA UFADHILI WA MASOMO YA SMZ NA MIKOPO YA ELIMU YA JUU kwa AWAMU YA PILI

MWAKA WA MASOMO 2021/22

 

·        WANAFUNZI WALIOTEULIWA KUPATA MIKOPO NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA VYUO VYA NDANI YA NCHI

·        WANAFUNZI WALIOTEULIWA KUPATA MIKOPO NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA VYUO VYA NJE YA NCHI

·        WANAFUNZI WALIOTEULIWA KUPATA MIKOPO NGAZI YA SHAHADA YA UZAMILI VYUO VYA NDANI YA NCHI

·        WANAFUNZI WALIOTEULIWA KUPATA MIKOPO NGAZI YA SHAHADA YA UZAMIVU VYUO VYA NDANI YA NCHI

 

WAOMBAJI WOTE WALIOTEULIWA KUPATA MKOPO PAMOJA WANATAKIWA KUZINGATIA YAFUATAYO:

 

·        KILA MWOMBAJI ALIYETEULIWA ATALAZIMIKA KUJAZA MKATABA AMBAO UTAJAZWA KWA KUTUMIA MFUMO WA ‘’ZOLAS’’ UNAOPATIKANA KATIKA AKAUNTI ZA WAOMBAJI WA MIKOPO. HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAYEFANYIWA MALIPO YA GHARAMA ZA MASOMO BILA YA KUJAZA MKATABA WA MIKOPO.

·        MWOMBAJI ALIYEPATA MKOPO KUTOKA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TANZANIA (HESLB) ATAFUTWA KATIKA ORODHA YA WAOMBAJI WALIOPATIWA MIKOPO NA BMEJZ ILI KUEPUSHA MWOMBAJI MMOJA KUPATA MIKOPO KUTOKA BODI ZOTE MBILI KWA WAKATI MMOJA KINYUME NA SHERIA.

·        MIKOPO INAYOTOLEWA NA BMEJZ KWA WAOMBAJI WAPYA WA MWAKA WA MASOMO 2021/22 HAIWAHUSU WAAJIRIWA WA TAASISI ZA UMMA ZA SMZ NA SMT. MWOMBAJI AMBAYE NI MWAJIRIWA NA JINA LAKE LIMEJITOKEZA KATIKA MAJINA YALIYOTANGAZWA ANAOMBWA ASIJAZE MKATABA NA BODI HAITOHUSIKA NA MADAI YOYOTE YA GHARAMA ZA MASOMO KATIKA CHUO ALICHOPATA UDAHILI.

·        WAOMBAJI WA WALIOTEULIWA KUPATA MIKOPO KWA VYUO VYA NJE YA MIKOPO WANATAKIWA KUCHAGUA AINA MOJA TU YA MKOPO WA ADA AU POSHO LA KUJIKIMU. GHARAMA NYENGINE ZOTE ZA MASOMO ZITALIPWA NA MNUFAIKA MWENYEWE

·        MUDA WA MWISHO WA KUJAZA MKATABA HUO WA MKOPO NI TAREHE 30 NOVEMBA, 2021.

·        MAJINA YA WAOMBAJI WA VYUO VYA NDANI WALIOTEULIWA YATAANZA KUTUMWA KATIKA VYUO HUSIKA KUANZIA TAREHE 11/11/2021

 

TANBIHI:

KWA UFAFANUZI WA SUALA LOLOTE LINALOHUSU MIKOPO PAMOJA NA NAMNA YA KUENDELEA NA UJAZAJI WA MIKATABA YA MIKOPO KWA KUTUMIA MTANDAO WASILIANA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR KWA KUFIKA MOJA KWA MOJA KATIKA OFISI ZAO ZILIZOPO KATIKA JENGO LA SINEMA YA MAJESTIKI VUGA ZANZIBAR NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI CHAKECHAKE PEMBA AU PIGA SIMU KWA KUTUMIA NAMBARI MAALUM ZIFUATAZO:

 

0777 348967 AU 0777348973