·
Kila mwajiri anapaswa kuijuilisha Bodi
mtumishi mpya anayeajiriwa ndani ya miezi mitatu ili Bodi ijiridhishe kama
mwajiriwa huyo ni mdaiwa wa Bodi au la.
·
Ikithibitika kuwa mwajiriwa ni mdaiwa wa
Bodi, mwajiri atapaswa kukata kiwango cha deni kutoka kwenye mshahara wa kila
mwezi wa mdaiwa kwa utaratibu ambao Bodi itaona unafaa.
·
Mwajiri atawajibika kuwasilisha mikato ya
mshahara wa kila mwezi wa mdaiwa si zaidi ya siku 15 za mwezi unaofuata kwa
utaratibu utakaotolewa na Bodi.
· Kwa
kukubali kumwajiri mdaiwa wa BMEJZ, mwajiri hatokuwa na nafasi ya kukwepa
wajibu wake wa kuanza kukata mshahara wa mdaiwa na kuwasilisha marejesho kwa
BMEJZ kwa kisingizio cha kutokuwa mshiriki katika mkataba wa mkopo kati ya
BMEJZ na mdaiwa.
Mwajiri
atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo anaweza kuchukuliwa hatua za
kisheria zifuatazo:
·
Kutozwa faini au tozo nyengine yoyote ile
ambayo Bodi itaona inafaa kwa kuchelewa kuwasilisha kwa wakati mikato ya
mshahara wa mdaiwa kwenye ofisi za Bodi (Kifungu cha 27(1) cha Sheria ya Bodi).
·
Kutozwa faini inayofikia shilingi milioni tano
au kufungwa jela kwa kifungo kisichopungua miezi 12 au adhabu zote mbili kwa
pamoja kwa kushindwa kukata deni la mdaiwa wa Bodi kutoka kwenye mshahara wake
na kuwasilisha mikato hiyo kwenye ofisi za Bodi (Kifungu cha 27(2) cha Sheria ya
Bodi).
·
Kulipa deni lote linalodaiwa pamoja na tozo
nyenginezo ambazo Bodi itaona zinastahiki kulipwa (Kifungu cha 27(3) cha Sheria ya
Bodi).