1.0 MUONGOZO WA UREJESHAJI
MIKOPO
Sheria
Namb. 3/2011 ya Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu Zanzibar kifungu cha 22(1)
(b) kimeeleza wajibu wa kila mnufaika wa mkopo unaotolewa na Bodi ya Mikopo
ya Elimu ya Juu Zanzibar (BMEJZ) kurejesha mkopo huo Serikalini kupitia (BMEJZ)
mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo au kabla ya hapo kadiri Bodi itakavyoona
inafaa.
Kila
mdaiwa ni lazima alipe deni lote analodaiwa na Bodi likijumuisha fedha
alizolipwa mkononi/au kupitia akaunti yake ya benki na zilizolipwa moja kwa moja
kupitia akaunti za Chuo alichosoma.
Mkopaji
anaweza kurejesha mkopo wake wote kwa pamoja au kwa kiwango maalum cha malipo
kwa mwezi ndani ya muda maalum uliowekwa na Bodi kulingana na kima cha mkopo
aliopewa.
1.1
Wajibu
wa Mkopaji
· Kutoa
taarifa kwa uongozi wa BMEJZ kuhusu kuhitimu masomo yake na kupata ajira.
· Kutoa
taarifa sahihi ziwemo anwani ya makazi, mwajiri au pahala pa kazi endapo
mkopaji atakuwa ni mjasiriamali.
· Kuanza
marejesho ya mkopo kwa kumtaka mwajiri wake kukata deni analodaiwa na BMEJZ
kutoka katika mshahara wake wa kila mwezi na kuwasilisha mikato hiyo ofisi za
Bodi kwa utaratibu ambao Bodi itaona unafaa.
·
Mdaiwa ambaye si muajiriwa atalipa mkopo wake
kwa kiwango maalum kwa mwezi ambacho atakubaliana na BMEJZ.
Endapo mkopaji atashindwa kurejesha mkopo baada ya
kufika kwa muda wa marejesho,
· Atalazimika
kulipa kiasi chote cha mkopo na gharama nyenginezo zinazoweza kutokea kutokana
na kukwepa kulipa mkopo wake ikiwa ni pamoja na tozo ya mawakili.
·
Bodi inaweza kumfikisha kwenye vyombo vya
sheria na kufungua mashtaka ya madai kwa mkopaji atakayekiuka wajibu wake wa
kulipa deni analodaiwa na Bodi.
·
Kutozwa faini isiyopungua shilingi 50,000 kwa
mwezi kwa kila marejesho ambayo hayatowasilishwa kwa wakati stahiki.
·
Bodi inaweza kuchukua hatua nyengine zozote,
kwa mujibu wa sheria, itakazoona zinafaa dhidi ya mdaiwa.
1.3
Muda
wa Marejesho
? Mkopaji
ambaye wakati wa kuomba mkopo hakuwa na ajira, anapaswa kuanza marejesho yake
baada ya kumalizika kipindi cha mwaka mmoja cha msamaha (grace period) tokea
kuhitimu masomo yake.
·
Mkopaji ambaye wakati wa kuomba mkopo alikuwa
ni mwajiriwa au amejiajiri, anapaswa kuanza marejesho ya mkopo mara tu baada ya
kuhitimu masomo yake au ndani ya muda wowote ambao Bodi itaona unafaa.
·
Mkopaji anapaswa kuendeleza mfululizo wa
marejesho ya mkopo wake ndani ya muda uliowekwa na BMEJZ bila ya kusita kwa
marejesho hata kwa mwezi mmoja. Hata hivyo Bodi inaweza kubadilisha muda wa
mwisho wa marejesho kulingana na kiwango cha deni, uwezo wa kulipa wa mkopaji,
utayari na uaminifu wa mkopaji kulipa deni lake, muda wa mkataba wa ajira
uliobaki kabla ya kustaafu.
1.4 Rufaa
kwa Wasiriodhika na Madeni yao
Mkopaji
ambaye hatoridhika na deni lake atakalokabidhiwa na Bodi baada ya kuhitimu
masomo yake anaweza kukata rufaa kwa kuomba kufanyika uhakiki mpya ya deni lake
kwa utaratibu ambao Bodi itaona unafaa. Muombaji mwenye haki ya kukata rufaa na
kusikilizwa ni yule ambaye:
a)
Ametoa taarifa kwa Bodi mara baada ya
kuhitimu masomo yake.
b)
Amewasilisha rufaa yake kimaandishi
akiambatisha na vielelezo vitakavyohitajika ndani ya siku 30 tokea tarehe
aliyopokea barua ya kumjulisha deni lake na inayomtaka kuanza taratibu stahiki
za kuanza marejesho ya mkopo wake.
c)
Barua yake ya rufaa inaonesha vipengele
anavyodai vipitiwe upya na Bodi.
d) Ameanza
kurejesha deni lake wakati anasubiri kutolewa maamuzi ya rufaa yake.