mersin escort porn

Kuanzia mwaka wa masomo 2016/17, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia BMEJZ imeanzisha utaratibu wa kutoa nafasi za ufadhili wa masomo (scholarships) kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika mitihani ya Taifa ya kidato cha sita.

Walengwa wa ufadhili wa masomo watakuwa wanafunzi wa kidato cha sita wa masomo ya sayansi wenye ufaulu mzuri zaidi katika mitihani yao ya taifa ya kidato cha sita. Kila mwaka kutatolewa nafasi kumi (10) kwa wanafunzi watakaotimiza sifa za kupatiwa ufadhili wa masomo wa SMZ.

Wanufaika wa ufadhili wa masomo wa SMZ hawatopaswa kurejesha gharama za masomo zilizotumika kwa ajili yao endapo watatimiza kikamilifu masharti ya ufadhili.

Utaratibu huu mpya umekusudiwa kuhamasisha ari ya ushindani wa kimasomo kwa wanafunzi wa kidato cha sita na hatimaye kuwawezesha kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya Taifa.

Sifa za waombaji wa Nafasi za Ufadhili wa Masomo za SMZ

Sifa zitakazozingatiwa wakati wa uteuzi wa waombaji wa nafasi za ufadhili wa masomo wa SMZ ni:

 • Muombaji awe Mzanzibari.
 • Yeye mwenyewe binafsi atajaza fomu ya maombi ya nafasi za ufadhili wa masomo wa SMZ.
 • Awe na ufaulu mzuri zaidi wa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi.
 • Awe amehitimu masomo ya kidato cha sita katika mwaka husika wakati wa kutuma maombi.
 • Awe mwanafunzi aliyehitimu masomo yake ya kidato cha sita kutoka skuli za sekondari za serikali au binafsi zilizopo Zanzibar.
 • Awe amepata udahili kwenye chuo cha elimu ya juu kilichopo Tanzania tu na kinachotambuliwa na mamlaka husika nchini.
 • Fani atakayosoma iwe miongoni mwa vipaumbele vya SMZ. Mwanafunzi akibadili fani chuoni ufadhili utafutwa na atapaswa kurejesha fedha zote zilizotumika baada ya kuhitimu.
 • Asiwe na mkopo au ufadhili wa masomo kutoka taasisi nyengine.
 • Awe tayari kujaza mkataba wa ufadhili wa masomo wa SMZ na kufuata kikamilifu masharti yote yaliyotajwa ndani yake.
Mafao ya Ufadhili wa Masomo wa SMZ

Ufadhili wa masomo wa SMZ unajumuisha mafao yatakayotolewa na BMEJZ kwa utaratibu wa awamu au mkupuo kulingana na mfumo wa masomo katika Chuo au Taasisi inayohusika au BMEJZ itakavyoona inafaa kulingana na uwezo wake. Mafao kwa wanufaika wa nafasi za ufadhili wa masomo wa SMZ yanajumuisha:

 • Ada kamili ya masomo kwa fani aliyoomba isiyozidi shs milioni 10 kwa mwaka.
 • Ada ya mitihani kwa asilimia 100.
 • Posho la kujikimu maisha shs 1,500,000/= kwa mwaka sawa na shs 750,000/= kwa kila muhula.
 • Gharama za vitabu shs 200,000/= kwa mwaka.
 • Malipo kwa mafunzo ya vitendo shs 300,000/=
 • Mahitaji maalum ya kitivo (special faculty requirements)
Utaratibu wa Malipo ya Ufadhili wa SMZ
 • Ada kamili mwaka italipwa chuoni moja kwa moja mara mbili kwa mwaka. Ada hii italipwa katika mwezi wa kwanza wa kila muhula baada ya mwanafunzi kuwasilisha ankara ya malipo (invoice).
 • Posho la kujikimu litalipwa kwa muhula kupitia akaunti ya mwanafunzi.
 • Posho la vitabu litalipwa mara moja kwa mwaka kupia akaunti ya mwanafunzi.
 • Posho la mafunzo ya vitendo na mahitaji maalum ya kitivo yatalipwa kupitia akaunti ya mwanafunzi baada ya kuwasilishwa kwa barua za chuo zinazothibitisha kulipwa kwa mafao hayo kwa mwanafunzi husika.
Masharti ya Nafasi za Ufadhili wa Masomo wa SMZ

Ufadhili wa masomo wa SMZ umeambatana na masharti ambayo kila mwanafunzi atakayepatiwa ufadhili huo atalazimika kuyatekelza kikamilifu. Miongoni mwa masharti hayo ni:

 • Mwanafunzi awe tayari kujaza mkataba wa ufadhili wa masomo wa SMZ na kufuata kikamilifu masharti yote yaliyotajwa ndani yake.
 • Mwanafunzi atalazimika kufanya kazi katika taasisi yoyote ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au katika taasisi nyengine yeyote kwa ridhaa ya SMZ baada ya kuhitimu masomo yake kwa muda usiopungua miaka minne. Iwapo mwanafunzi hatokuwa tayari kufanya kazi Zanzibar au kufanya kazi pahala pengine bila ya ridhaa ya SMZ, mwanafunzi husika atalazimika kuilipa BMEJZ gharama zote za masomo zilizotumika kugharamia masomo yake. Pia atalazimika kulipa ziada ya asilimia 15 ya gharama zote zilizotumika ikiwa ni adhabu.
 • Kila mwanafunzi atalazimika kuwa na wadhamini wasiopungua wawili wataokubali kuchukuwa jukumu la kuhakikisha mwanafunzi anarejea Zanzibar baada ya kumaliza masomo yake na kufanya kazi kwa muda usiopungua miaka minne. Aidha, wadhamini watarejesha gharama zote za masomo kama ilivyoelezwa katika kifungu nambari 2.2 hapo juu endapo mwanafunzi huyo hatorejea Zanzibar.
 • Endapo mwanafunzi atakuwa miongoni mwa wanufaika wa mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu ya Juu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (HESLB), mwanafunzi huyo atalazimika kuacha mkopo huo.
 • BMEJZ inaweza kubadilishana taarifa za mwanafunzi na taasisi nyengine zinazotoa mikopo au nafasi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili taasisi hizo zizuie utoaji wa mikopo kwa mnufaika wa nafasi za ufadhili wa masomo zinazotolewa na SMZ.
Wajibu wa Mwanafunzi Aliyepata ufadhili wa Masomo wa SMZ
 • Kuijulisha BMEJZ kuhusu mabadiliko yoyote yale yanayoweza kuathiri masomo yake na ufadhili wake wa masomo kwa namna yoyote ile.
 • Kuipatia BMEJZ taarifa nyengine zozote zile zinazohusiana na nafasi yake ya ufadhili wa masomo pale atakapotakiwa kufanya hivyo.
 • Atawajibika kutuma matokeo yake ya mitihani kwa BMEJZ kila anapomaliza mwaka wa masomo pamoja na kuwasilisha nakala ya shahada yake baada ya kuhitimu masomo yake na kurudi nyumbani.
 • Kutuma Ankara ya malipo (invoice) kutoka Chuo/Taasisi yake ya masomo kwa BMEJZ ili aweze kufanyiwa malipo. Pia mwanafunzi atawajibika kuleta risiti za malipo kila baada ya muhula wa masomo na kusaini fomu maalum ya malipo.
 • Anawajibika wakati wote wa kipindi cha masomo kuheshimu na kutii sheria ndogo ndogo za chuo, kanuni na maelezo yatolewayo mara kwa mara.
 • Kukamilisha mkataba mpya wa nafasi ya ufadhili wa masomo kila mwaka kwa muda wote ambao mwanafunzi atakuwa anaendelea na masomo.
Usitishaji wa Ufadhili wa Masomo wa SMZ

BMEJZ inaweza kusitisha nafasi ya ufadhili wa masomo kwa mwanafunzi ikiwa:

 • Mwanafunzi atashindwa kuendelea na masomo kwa kutofaulu au kuacha masomo kwa sababu yoyote ile.
 • Mwanafunzi atabadilisha chuo au fani bila ya kutoa taarifa na kuridhiwa na BMEJZ.
 • Mwanafunzi kutuma maombi ya kusitisha ufadhili wa masomowa SMZ.
 • Mwanafunzi atapata udhamini wa masomo kutoka taasisi nyengine kwa madai yanayolingana ikiwa BMEJZ imelipa/haikulipa sehemu/ukamilifu wa madai hayo.
 • Itabainika kuwa mwanafunzi anajihusisha na vitendo vya uhalifu, kufukuzwa chuo au BMEJZ kupokea taarifa isiyoridhisha kutoka taasisi anayosoma.

Upcoming events