1. Wajibu wa Mdhamini wa Mkopaji
Mdhamini
wa mkopaji anawajibika:
· Kutoa
taarifa kwa Bodi kuhusu kumaliza masomo na/au kupata ajira kwa mkopaji.
· Kutoa
taarifa sahihi za mkopaji zikiwemo anwani ya makazi, mwajiri au pahala pa kazi
endapo mkopaji atakuwa ni mjasiriamali.
· Kumshajiisha
mkopaji kulipa deni lake kwa wakati kwa utaratibu uliopangwa na Bodi.
·
Kulipa deni endapo mdaiwa atakwepa kulipa
deni kwa hiari na kutotekeleza masharti ya marejesho ya mkopo. Aidha, mdhamini
au mtu mwengine yeyote (wakala) anaweza kumlipia mkopaji deni lake kwa hiari.
2. Adhabu kwa Mdhamini anayekiuka wajibu wake
Mdhamini atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake
ipasavyo anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kama ifuatavyo:
·
Kutozwa
faini inayofikia shilingi milioni 5 au kufungwa jela kwa kifungo kisichopungua
miezi 12 au adhabu zote mbili kwa pamoja kwa kushirikiana na mdaiwa kukwepa
kulipa deni analodaiwa. (Kifungu cha 27(2) cha Sheria ya Bodi).
· Kulipa deni lote linalodaiwa pamoja na tozo
nyenginezo ambazo Bodi itaona zinafaa kulipwa (Kifungu cha 27(3) cha Sheria ya
Bodi).