Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inawatangazia wanafunzi wote wanaohitaji kujiendeleza katika fani mbali mbali za Elimu ya Juu kuwa inatoa nafasi kwa awamu ya pili ya uchukuaji wa fomu za maombi ya mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Fomu za maombi zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 21/09/2018 hadi tarehe 28/09/2018.

Mikopo itatolewa kwa waombaji waliotimiza sifa za kujiunga na masomo ya Elimu ya Juu katika ngazi za:-
1.    Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree)
2.    Shahada ya Pili (Master Degree)
3.    Shahada ya Tatu (PhD)

Walengwa wa Maombi ya Mikopo ni:-
1.    Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
2.    Wahitimu wa Diploma wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
3.    Wahitimu wa Shahada ya Kwanza wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Pili.
4.    Wahitimu wa Shahada ya Pili wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Tatu.

Waombaji wa mikopo wanapaswa kuzingatia fani za vipaumbele vya Serikali ambazo zinapatikana katika tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (www.moez.go.tz) na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (www.zhelb.go.tz)
Fomu za maombi ya mikopo zitalipiwa ada ya shilingi 10,000 ambazo zitalipwa moja kwa moja na muombaji kwenye akaunti namba 021108001357 ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyopo katika Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Wanaohitaji fomu za maombi ya mikopo wanaombwa kufika katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu zilizopo Vuga jengo la Majestik sinema kwa Unguja na jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, ChakeChake Pemba.

Waombaji wa mikopo wanatakiwa kuchukua nyaraka zifuatavyo:-
1.    Kitambulisho cha Mzanzibari.
2.    Fomu ya malipo (Pay Slip) kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
3.    Vivuli vya vyeti na matokeo ya masomo kwa ngazi aliyohitimu.

Waombaji wote wanakaribishwa.Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inawatangazia wanafunzi wote wanaohitaji kujiendeleza katika fani mbali mbali za Elimu ya Juu kuwa inatoa nafasi kwa awamu ya pili ya uchukuaji wa fomu za maombi ya mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Fomu za maombi zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 21/09/2018 hadi tarehe 28/09/2018.

Mikopo itatolewa kwa waombaji waliotimiza sifa za kujiunga na masomo ya Elimu ya Juu katika ngazi za:-
1.    Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree)
2.    Shahada ya Pili (Master Degree)
3.    Shahada ya Tatu (PhD)

Walengwa wa Maombi ya Mikopo ni:-
1.    Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
2.    Wahitimu wa Diploma wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
3.    Wahitimu wa Shahada ya Kwanza wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Pili.
4.    Wahitimu wa Shahada ya Pili wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Tatu.

Waombaji wa mikopo wanapaswa kuzingatia fani za vipaumbele vya Serikali ambazo zinapatikana katika tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (www.moez.go.tz) na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (www.zhelb.go.tz)
Fomu za maombi ya mikopo zitalipiwa ada ya shilingi 10,000 ambazo zitalipwa moja kwa moja na muombaji kwenye akaunti namba 021108001357 ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyopo katika Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Wanaohitaji fomu za maombi ya mikopo wanaombwa kufika katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu zilizopo Vuga jengo la Majestik sinema kwa Unguja na jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, ChakeChake Pemba.

Waombaji wa mikopo wanatakiwa kuchukua nyaraka zifuatavyo:-
1.    Kitambulisho cha Mzanzibari.
2.    Fomu ya malipo (Pay Slip) kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
3.    Vivuli vya vyeti na matokeo ya masomo kwa ngazi aliyohitimu.

Waombaji wote wanakaribishwa.