Bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar (bmejz) inatangaza nafasi za masomo ya shahada ya kwanza ya  uandishi wa habari katika chuo kikuu cha zhejiang cha nchini china katika mwaka wa masomo 2018/19. Sehemu ya gharama za masomo zitakuwa ni mkopo unaopaswa kurejeshwa baada ya kumaliza masomo.

Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa wawe na sifa zifuatazo:

  1. Waweze kuzungumza na kuandika lugha ya kichina.
  2. Wawe wamemaliza kidato cha sita au diploma ya uandishi wa habari.
  3. Wawe na umri usiozidi miaka 25 ifikapo septemba 2018.
  4. Wawe na afya njema.
  5. Wawe wazanzibari.
  6. Wawe tayari kufanyiwa usaili wa lugha ya kichina

Barua za maombi ziambatanishwe pamoja na:

  1. Vivuli vya vyeti vya masomo na matokeo ya mitihani kwa ngazi husika aliyohitimu muombaji kikiwemo cheti cha kidato cha nne.
  2. Kivuli cha kitambulisho cha mzanzibari.
  3. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  4. Kivuli cha hati ya kusafiria

Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti za bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar (www.zhelb.go.tz) na wizara ya elimu na mafunzo ya amali (www.moez.go.tz).

Barua na fomu za maombi zilizokamilika ziwasilishwe katika ofisi za bodi ya mikopo ya elimu ya juu zilizopo vuga unguja na chakechake pemba si zaidi ya tarehe 20 julai, 2018.

     Application form