Bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar (bmejz) inatangaza nafasi za masomo ya shahada ya kwanza kupitia ufadhili wa serikali ya Ras Al-Khaymah kwa mwaka wa masomo 2018/19.

Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa wawe na sifa zifuatazo:

  1. Wawe wamemaliza kidato cha sita mwaka 2018 na kupata ufaulu wa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi.
  2. Wawe na umri usiozidi miaka 22 ifikapo septemba 2018.
  3. Wawe na afya njema.
  4. Wawe wazanzibari.
  5. Wawe tayari kufanya mitihani ya kupiwa uwezo wa lugha ya kiingereza (toefl au ielts)

Barua za maombi ziambatanishwe pamoja na:

  1. Vivuli vya vyeti vya masomo na matokeo ya mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita .
  2. Kivuli cha kitambulisho cha mzanzibari.
  3. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  4. Kivuli cha hati ya kusafiria

Barua za maombi ziwasilishwe katika ofisi za bodi ya mikopo ya elimu ya juu zilizopo vuga unguja na chakechake pemba si zaidi ya tarehe 20 julai, 2018.