Bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar (bmejz) inatangaza nafasi za masomo ya shahada ya kwanza kupitia ufadhili wa benki ya maendeleo ya kiislamu kwa mwaka wa masomo 2018/19.

Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa wawe na sifa zifuatazo:

  1. Wawe wamemaliza kidato cha sita mwaka 2018 na kupata ufaulu wa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi.
  2. Wawe na umri usiozidi miaka 22 ifikapo septemba 2018.
  3. Wawe tayari kujiunga na vyuo husika katka nchi za uturuki na malaysia
  4. Wawe na afya njema.
  5. Wawe wazanzibari.

Barua za maombi ziambatanishwe pamoja na:

  1. Vivuli vya vyeti vya masomo na matokeo ya mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita .
  2. Kivuli cha kitambulisho cha mzanzibari.
  3. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  4. Kivuli cha hati ya kusafiria

Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti za bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar (www.zhelb.go.tz) na wizara ya elimu na mafunzo ya amali (www.moez.go.tz).

Barua na fomu za maombi zilizokamilika ziwasilishwe katika ofisi za bodi ya mikopo ya elimu ya juu zilizopo vuga unguja na chakechake pemba si zaidi ya tarehe 20 julai, 2018.

  Anouncement Poster 

  Application Form