Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inatangaza nafasi za ufadhili wa masomo kwa njia ya scholarship zinazotolewa na Serikali ya Oman kwa vijana waliofaulu vizuri zaidi mitihani yao ya kidato cha sita kwa mwaka 2018 na  kufanikiwa kupata ufaulu wa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi.

Masharti ya kuomba nafasi hizo ni:

  • Muombaji awe ni Mzanzibari
  • Awe amehitimu kidato cha sita katika skuli za Sekondari za Zanzibar.
  • Awe amefaulu vizuri masomo ya sayansi au biashara kwa kiwango cha daraja la kwanza.
  • Awe tayari kusoma fani zinazohusiana na uhandisi, biashara au fedha katika vyuo vilivyopo Oman.
  • Awe na umri usiozidi miaka 24 ifikapo Oktoba 2018.
  • Awe na afya njema
  • Baada ya kuhitimu atapaswa kurudi nyumbani na kufanya kazi Zanzibar kwa kipindi kisichopungua miaka minne.

Fomu za maombi ya scholarship hizo zinapatikana katika tovuti za Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (www.moez.go.tz).

Fomu za maombi zinapaswa kuambatishwa na:

  • Kivuli cha kitambulisho za Mzanzibari.
  • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  • Kivuli cha cheti cha kidato cha nne.
  • Kivuli cha cheti/matokeo ya mitihani (result slip) ya kidato cha sita.
  • Ithibati ya tabia njema (Certificate of good conduct) kutoka skuli aliyomalizia masomo.
  • Taarifa ya uchunguzi wa afya (medical report).
  • Picha sita za passport size.
  • Kivuli cha hati ya kusafiria (Passport).

Kwa waombaji waliopo Unguja, barua na fomu za maombi zilizojazwa kikamilifu ziwasilishwe ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyopo jengo la Majestic Cinema, Vuga. Waombaji waliopo Pemba wawasilishe maombi yao katika Afisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu zilizopo katika jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Chakechake.

Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya IJUMAA ya tarehe 14/09/2018 saa 9:30 mchana.

   OMAN SCHOLARSHIPS 2018 APPLICATION FORMS