Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu - Zanzibar inatangaza nafasi za masomo nchini India kwa ngazi ya shahada ya kwanza, ya pili na ya tatu kwa mwaka wa masomo 2018/2019 katika fani za Uhandisi, Sheria, Sayansi, Mitindo na Mavazi, Uongozi na Uandishi wa Habari.

Sifa za Muombaji
  1. Awe Mzanzibari.
  2. Kwa waombaji wa shahada ya kwanza wawe:-
    • Wamehitimu masomo ya kidato cha sita na kupata alama za ufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza tu na wawe na umri usiozidi miaka 40. AU
    • Wamehitimu masomo ya Diploma na kupata alama za ufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili na wawe na umri usiozidi miaka 40.
  3. Waombaji wa shahada ya uzamili (Master Degree) Wawe wamehitimu masomo ya Shahada ya Kwanza na kupata alama za ufaulu kwa kiwango cha daraja la pili la juu na wawe na umri usiozidi miaka 45.
  4. Waombaji wa shahada ya uzamivu (PhD) Wawe wamemaliza masomo ya Shahada ya Pili na kupata alama za ufaulu kwa kiwango cha daraja la pili la juu na wawe na umri usiozidi miaka 47.
Taratibu za Maombi

Waombaji watalazimika kujaza fomu za maombi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. (www.moez.go.tz) na (www.zhelb.go.tz) pamoja na sifa za kudahiliwa.

Fomu za Maombi ziambatanishwe na vyeti vya mitihani ya Taifa, cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha Mzanzibari na ziwasilishwe kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, si zaidi ya tarehe 18 Mei, 2018.

Kwa walioko Pemba fomu za maombi ziwasilishwe kwa Mratibu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar katika ofisi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Chake Chake Pemba.